Menu
 


Baadhi ya wananchi waliobahatika kupata mafuta katika kituo cha ORXYambacho kilikua kinauza lita tano tano kwa kila mmoja. (Picha na Mbeya Yetu)
*****
Na mwandishi wetu.
 Baadhi ya vituo vya mafuta jijini Mbeya vimegoma kuuza mafuta aina ya Petroli sababu ya kupinga hatua ya EWURA kupunguza bei ya mafuta mara kwa mara.

Wakiongea na mwandishi wa habari hii baadhi ya wafanyakazi wa vituo vya mafuta vya ORXY na GAPCO ambao hawakutaka majina yao yatajwe redioni wamesema si kwamba mafuta hayopo kwenye vituo vyao bali vimefungwa kutokana na mabadiliko ya bei yanayofanywa na EWURA mara kwa mara.

Aidha wamesema endapo wamengepewa siku 7 za kuuza mafuta waliyokuwa nayo ndipo waanze kuuza bei mpya tatizo la mafuta lisingekuwepo.

Bei ya mafuta aina ya Petroli kwa sasa ni 2200 kwa lita wakati awali ilikuwa ni shilingi elfu kwa lita

Kutokana na tatizo hilo la mafuta aina ya Petroli Bomba Fm imewashuhudia mamia ya watu wakipanga foleni ndefu kwa ajili ya kwenda kununua mafuta hata hivyo kila mteja hupewa mafuta yasiyozidi lita tano.

Post a Comment

 
Top