Menu
 

Na mwandishi wetu.
Wananchi wa kata ya Iwambi jijini Mbeya wamemhamisha kwa nguvu Bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Twagire wakimtuhumu kuhusika na ushirikina.

Uamuzi huo umefikiwa jioni katika kikao cha kata kilichofanyika kwenye ukumbi wa kata ya Iwambi ambapo bibi huyo anadaiwa kuhusika na mauaji ya watoto watatu kwa imani za kishirikina.

Afisa mtendaji wa kata hiyo Jackobo Sanga amesema uamuzi wa kumwamisha kinguvu bibi huyo umefikiwa ili kulinda usalama wake baada ya baadhi ya wananchi kuonesha kuchukizwa na vitendo vya bibi huyo.

Baadhi ya wakazi wa kata hiyo ambao hawakupenda majina yao kutajwa redio wamesema si mara moja bibi huyo kuamishwa katika maeneo mbalimbali ya jiji ambapo mara ya kwanza bibi huyo alihamishwa kutoka Mbalizi na Nzovwe jijini hapa.

Post a Comment

 
Top