Menu
 

Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya likiwemo tukio la kwanza lililotokea, mtaa wa Ilolo Igoma "A" kata ya Isanga jijini Mbeya ambapo mtoto aitwaye Ivon Mwakyusa (3) amekutwa amekufa katika shimo la choo.

Tukio hilo la mtoto kufariki limetokea katika choo kinachomilikiwa na Bwana Robert Edson Mwambegere (29) ambapo ni umbali wa mita 50 kutoka anyumbani alipokuwa akiishi na wazazi wake.

Mzazi wa mtoto huyo Bwana Upendo Mwakyusa amesema mwanae alitoweka nyumbani majira ya saa 8 mchana, Novemba 20 mwka huu na mara baada ya kupotea kwa mtoto huyo taarifa ilitolewa sehemu mbalimbali vikiwemo vituo vya Redio lakini bila mafanikio hadi majira ya saa mbili alipokutwa amefariki katika shimo hilo la choo.

Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Juma Kahawa alitoa taarifa Kituo cha Polisi ambapo Polisi walifika na kuuchukua mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Rufaa jijini hapa kwa uchunguzi zaidi.

Hili ni tukio la pi9li kutokea kwa mawaka huu katika mtaa huo wa Igoma A, ambapo mwezi Mei mtoto mwingine alikutwa amefariki katika kisima cha maji kinachomilikiwa na Bwna Juma Kahawa ambaye ni mwenyekiti wa mtaa huo.
Kutokana na kukerwa na matukio hayo wananchi wa mtaa huo waliamua kufanya mkutano wa hadhara kulaani vikali vitendo hivi vimavyohusishwa na imani za kishirikina na kuamua kuendesha zoezi la upigaji kura za maoni ambapo jumla ya kura 150 zilipigwa, na kura 9 ziliharibika, huku kura 1 ili mtaja mama mmoja, Kura 20 zilimdondokea Mganga wa tiba ya jadi na kura 120 zilimtaja kiongozi mmoja wa kijijini hapo.

Hata hivyo walioweza kupigiwa kura hawakuwepo katika mkutano na Damian Matipa na azimio la wananchi hao ni kuwa watu hao hawatakiwi kuwepo kijijini hapo kutokana na kujihusisha na mambo ya kishirikina, ndipo wananchi waliamua kuandama kwenda Kituo cha Polisi Mwanjelwa jijini hapa kushikiza watuhumiwa hao kuhamaeneo hilo.

Aidha katika kijiji cha Igoma "I" wilayani Mbeya vijini mwanaume asiyefahamika jila wala makazi, na umri unaokadiliwa kati ya 30 hadi 40 ameuwawa kwa kupingwa vitu butu kichwani na mwananchi wenye hasira kali  majira ya saa 7 mchana ndani ya nyumba ya Selina Sanga (28).

Chanzo cha kifo hicho ni kutokana na wivu wa kimapenzi kwani marehemu alikwenda kumsalimia mpenzi wake Selina na kumkuta mwanaume mwingine ndani ndipo Selina alipiga kelele za kuvamiwa ndipo kundi la wananachi wenye hasira kali kumshambulia hadi kufa mwanaume huyo.

Selina Sanga ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Igoma amekamatwa na Jeshi la polisi mkoani hapa kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya rufaa jijini hapa.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kwamba jeshi la polisi linafanya uchunguzi wake.

Post a Comment

 
Top