Menu
 

Watu wanne waliofariki wilayani Mbozi katika matukio matatu tofauti tukio la kwanza watu wawili wafariki baada ya kupigwa na radi katika kijiji cha Hatelele juzi majira ya saa tisa alasiri ambapo Bwana John Kibona (38) na Musa Mwakasamba (40) walipingwa na radi wakati wakienda kuwafuata watoto waliokuwa makichunga ng'ombe kutokana na mvua kubwa kunyesha ikiambatana na radi.

Tukio la pili katika kijiji cha Ilangali kata ya Isansa Juma Watson Mwashiuya (43) alifariki kwa kujinyonga na kamba ya katani baada ya kugundua anaishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU).

Hata hivyo marehemu mpaka anafikia hatua ya kujinyonga mkewe alikuwa hayupo nyumbani hapo.

Tukio la tatu katika kitongoji cha Mlowo kata ya Mlowo majira ya saa mbili kasorobo, mwana mke asiyefahamika alimtupa mtoto wa kiume umri wa siku moja katika mfuko wa rambo na kisha kutupa mtoni ambapo uliokotwa na wasamalia wema licha ya mtoto huyo kufariki dunia.

Balozi wa mtaa huo Bwana Thadeo Mwakapalila kwa kushirikiana na wananchi aliongoza mazishi kuuzika mwili wa mtoto huo huku wakifanya juhudi kwa kushirikiana kumtafuta mwanamke aliyehusika na unyama huo.

Post a Comment

 
Top