Menu
 


Na mwandishi wetu.
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya likiwemo tukio la mtu mmoja kuuawa kwa kuchomwa moto akiwa ndani ya nyumba yao kutokana na wivu wa kimapenzi.

Akiongelea matukio hayo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amesema kijana Mpumo Madirisha mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Ugunyambelele kata ya mkola wilayani Chunya mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya nyumba yao kuchomwa moto akiwa ndani  kutokana na wivu wa kimapenzi.

Amesema jeshi la polisi linawashikilia Bahati Mtungwa mwenye umri wa miaka 17 na Kwandu Matondo mwenye umri wa miaka 17 wote wakazi wa kijiji cha Ugunyambelele kwa tuhuma za kuhusika na tukio.

Aidha amesema kuwa tukio jingine limetokea kijiji cha Isangu kitongoji cha Shanko wilayani Mbozi ambapo Lavu Msala mwenye umri wa miaka 40 amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na watu wasiofahamika.

Hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa na Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Post a Comment

 
Top