Menu
 


Mbunge wa mstaafu wa Jimbo la Ileje ambaye pia ni Kamanda wa UVCCM wilaya ya Ileje Mheshimiwa Gideon Cheyo amesema kiongozi ataheshimiwa kwa matendo yake, wala si kwa heshima au cheo chake bali ni katika  hali ya kuwajibika kwa wananchi waliompa dhamana ya Uongozi.
 Katibu wa UVCCM mkoani Mbeya Bwana Ramadhani Kizinga amewataka makatibu wa UVCCM wa wilaya zote mkoani Mbeya kufanya kazi kwa bidii na maadili na kanuni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), vinginevyo watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Mbeya Dokta Stephen Mwakajumilo, amewataka vijana wa UVCCM kutotumiwa kama watu wa kuwawezesha watu wasiokuwa na sifa kuingia madarakani na hivyo kutosimamia sera madhubuti za Chama Cha Mapinduzi na serikali yake.
Baadhi ya wanachama Baraza la Vijana UVCCM wilaya ya Ileje mkoani Mbeya wakimsikiliza Kamanda wa UVCCM mkoa wa Mbeya Dr. Stephen Mwakajumilo katika Ukumbi wa CCM wilayani humo.

Post a Comment

 
Top