Menu
 

Na Ezekiel Kamanga, Ipinda Kyela.
Bwana Angolwisye Mwankotwa (40) amefumanikiwa akifanya tendo la ndoa na mke wa mtu aitwaye Bi Tulinangwe Kibinga (34) majira ya saa sita mchana jana, ambapo mume wa mke huyo alikuwa ibadani katika kanisa la Mount Zion Tabernacle Mission kujiji cha Bukinga wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Fumanizi hilo limetokea mara baada ya mume wa Bi Tulinangwe anayefahamika kwa jina la Bwana Afrika Mwakisisya kuoteshwa kuwa mkewe akifanya ngono nje ya ndoa na mwanaume mwingione, ndipo alipoondoka ghafla kanisani na kuwakuta mkewe na Bwana Angolwisye wakizini pasipo kufunga mlango wakiwa watupu.

Tukio hilo ni la pili kwa watuhumiwa hao, ambapo mwezi  Machi, mwaka huu, walikutwa wakizini katika shamba linanlomilikiwa na Bwana Afrika ambaye ni mume wa mwanamke huyo majira ya saa tatu asubuhi.

Aidha Bwana  Angolwisye Mwankotwa (40), alifiwa na mkewe miaka miwili iliyopita ambapo dada yake aitwae Bi Maria Ezekiel alishuhudia tukio hilo la aibu huku kaka yake akiwa ameshika nguo mkononi baada ya fumanizi hilo.

Hata hivyo mwanamke aliyefumaniwa Bi Tulinangwe ameaswa mara nyingi kuachana na mwanamme huyo na kukaidi kuwa hana mahusiano naye, lakini kakutwa akifanya ngono na mwanaume huyo pasipo woga na aibu yoyote licha ya mwanamke huyo kufanikiwa kuzaa watoto wa tano na mume wake wa ndoa Bwana Afrika.

Tukio hilo lilishuhudiwa na diwani wa kata ya Muungano Bwana Absalom Mwasipu ambapo kwa pamoja waliamua kumtoza mgoni Bwana Angolwisye faini ya shilingi laki tatu kama adhabu, ambazo mgoni ameahidi kuzilipa siku za usoni.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la  Mount Zion Tabernacle Mission Bwana Alphonce Danken Mwamakunge amesikitishwa na kitendo hicho cha aibu ambacho amekifanya mwanaume huyo kuingilia ndoa ya mtu, hali inayohatarisha amani hasa ukizingatia kipindi hiki kuna maladhi mengi yakiwemo magonjwa ya zinaa.

Post a Comment

 
Top