Menu
 

Watu watatu wamefariki dunia katika ajali ya barabarani mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Chapwa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, majira ya saa tatu usiku.

Gari namba AAV 9849 aina ya Toyota Cerica iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Malundu Mofya (38) raia wa nchi ya Zambia ambaye alifariki papo hapo pamoja na abiria wake wawili ambao nao ni walifariki kuwa ni Nickson Sirungwe (40) na Febinand Hayola (25) ambaye ni raia wa Tanzania, mkazi wa mji mdogo wa Tunduma.

Chanzo cha ajali hiyo ni kwamba gari hiyo ikiwa katika mwendokasi iligonga gari ya mizigo(roli) aina ya Scania yenye namba za usajili T 151 ABM iliyokuwa na tela namba T 504 APQ iliyokuwa inaendeshwa na dereva aitwaye Satinda Soghal (53), mkazi wa mkoani Iringa.

Hata hivyo miili yote ya marehemu hao imechukuliwa na ndugu zao  kwa ajili ya mazishi ambapo wanaume wawili raia wa Zambia wamesafirishwa kwenda Nakonde Zambia.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaasa madereva kuwa makini wawapo barabarani.

Post a Comment

 
Top