Menu
 

Watu watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso, hapo jana katika eneo la Mahenje wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo la abiria lenye nambari za uzajili T 173 AWF lilolokuwa likiendeshwa na dereva Stanley Sengo (30) ambalo liligongana uso kwa uso na gari la mafuta lenye nambari za usajili T 606 BKL aina ya Scania lenye tela namba T 357 BBV.

Tukio hilo la jali limetokea majira ya saa kumi na moja na dakika arobaini na tano za jioni, ambapo dereva wa gari dogo la abiria alipokuwa amepigwa na jua usoni  alipojaribu kukinga jua hilo kwa kutumia mkono gari lake lilihama njia na kuingia upande wa roli ambapo watu watatu walifariki dunia akiwepo mwanamke mmoja na wanaume wawili ambapo majina yao hayakuweza kufahamika mara moja.

Haya hivyo mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gabriel Kimolo alitembelea eneo la tukio pamoja na majeruhi hospitalini na kuwaasa madereva kuwa makini wawapo barabarani hasa katika msimu huu wa sikukuu kwa kuthamini utu wa abiria, kuepuka mwendokasi na ulevi.

Post a Comment

 
Top