Menu
 

Stendi ya magari ya abiria maarufu kama Daladala.Kabwe Mwanjelwa jijini Mbeya.
*****
Na mwandishi wetu.
Jeshi la polisi kikosi cha usalama wa barabarani mkoani Mbeya limewataka madereva kuhakikisha anatembea na leseni yake binafsi ili kurahisisha kupatikana kwa leseni zilizoisha muda wake.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha usalama wa barabarani Ezekiel Mgeni wakati wa mahojiano na mwandishi wetu mkoani hapa.

Amesema kwa yeyote atakayekamatwa hana leseni gari lake litakamatwa na kufikisha kituo cha polisi na hapatakuwa na adhabu yoyote kwa madereva hao mpaka pale atakapo peleka leseni yake.

Hata hivyo Kamanda MGENI amewaasa madereva kuwa makini, kufuata maadili na kanuni za  barabarani katika msimu huu wa sikukuu ya mika 50 ya Uhuru na ile Krismas na mwaka mpya  ili kunusura ajali kutokana uendeshaji magari yao ovyo na mwendokasi.

Post a Comment

 
Top