Menu
 

Mgeni rasmi wa mahafali ya 11 ya chuo cha Ufundi (MVTC) kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi  Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gabriel Kimolo akipokea zawadi ya samani, aina ya meza iliyobuniwa na kutengeneza na wahitimu hao katika mahafali  yaliyofanyika Desemba 16 mwaka huu, katika Ukumbi wa Chuo hicho eneo la Kadege, Forest ya zamani jijini Mbeya. 
 *****
Habari na Mtandao huu.
 Wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Kanisa la Moravian Tanzania(MVTC) Jimbo la Kusini Magharibi, Mkoani Mbeya wametakiwa kutumia weledi wao walioupata chuoni hapo kwa mandeleo ya Tanzania.
 
Akihutubia katika Mahafali ya 11 ya Chuo cha Ufundi, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Gabriel Kimolo amesema wahitimu wengi hapa nchini wanapimaliza elimu zao huonekana kuwa na vyeti vya nguvu lakini ukifuatilia utendaji wao kazi ni mdogo.

Mheshimiwa Kimolo amesema, inapofikia hatua hiyo jamii hujikuta katika lindi la umaskini kutokana na kuwa na watu wengi wamesoma lakini utendaji wao ni mdogo.

Pia Kimolo amesema makampuni mengi ya nje yamefikia mahali pa kuajiri watu wa kutoka makwao na sio watanzzania kutokana na juhudi na ufanisi katika kazi hizo na kuwaacha watanzania wakilalama kwa njaa ya ajira.

Hata hivyo amelitaka Kanisa la Moravian Tanzania kama kweli lina nia ya dhati ya kuisaidia jamii ya watanzania basi inapaswa kupanua chuo hicho kwa kuomba maeneo mengine ili kusongeza huduma kwa wananchi.

Aidha amelitaka kuomba ekari zaidi ya 100 ili kuweza kuikidhi haja ya kuwasaidia watanzania wa leo na wa kizazi kijacho badala ya kuwaachia wawekezaji wa nje maeneo makubwa ya ardhi kwa uwekezaji wa makampuni yao.

Mahafali hayo ni ya 11 ambapo wahitimu 167, wavulana 61 na wasichana 106 ambapo Mkuu wa Wilaya huyo amewakabidhi tuzo wanafunzi waliofanya vizuri katika kadhia mbalimbali ikiwemo nidhamu, usafi, masomo ya uhazili.
 
 Mkuu wa Chuo cha Ufundi(MVTC) kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Bwana Gurd Lwinga akitoa utambulisho katika mahafali ya 11 ya wahitimu wa chuo hicho yaliyofanyika Desemba 16 mwaka huu, katika Ukumbi wa Chuo hicho eneo la Kadege, Forest ya zamani jijini Mbeya amesema chuo hicho hutoa mafunzo ya Ushonaji nguo, Useremala, utengenezaji wa Umeme wa sola, umeme wa majumbani, uhaziri, hoteli, kompyuta na kozi za lugha ya kiingereza. 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa  VETA kanda ya nyanda za juu kusini Bwana Justine Luta amewataka wahitimu kwenda kutangaza vema sifa ya chuo hicho kwa kuhudumia vizuri wateja na kutengeneza samani bora zenye kuvutia na serikali inaunga mkono juhudi zinazofanya na kanisa la Moravian kwa juhudi wanazozitoa kwa vijana kuwapa mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa vyuo vingine vinavyomilikiwa na Veta.

Naye Katibu mkuu wa Kanisa la Moravian Mchungaji Daudi Msweve, amesema kanisa lake linawawezesha kupata vitendea kazi wanavyuo wanaohitimu ambapo jana walitoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 5,638,000 kwa wahitimu 167. 

Chuo hicho kimesajiliwa mwaka 2000 kikianza na wanafunzi 16 na namba ya usajili ni VTC/323/2002 na hakina ubaguzi wa dini, ukabila na ujinsia. Pia kuna asasi ambazo huleta watoto yatima kupewa mafunzo kama vile YWCA, NSALAGA na OAK - TREE ambazo husaidia kupunguza wimbi la watoto wa mitaani.

Post a Comment

 
Top