Menu
 

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mchungaji wa Kanisa la House Of  Prayer Bwana Seleman Liduke (51) lililoko kijiji cha Kapunga, kata ya Mapogoro wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya amefariki dunia majira ya saa 12 jioni hapo jana katika kitongoji cha Kapunga Site one  wilayani humo.

Mchungaji Liduke alikutwa na maafa hayo alipokuwa shambani kwake, baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi ambapo ilipokuwa inanyesha alijisetiri katika kibanda cha kuhamia ndege ndipo radi iliyoambatana na ngurumo kubwa ilimpiga mchungaji huyo usoni na kusababisha kuvunja damu mdomoni na puani na nguo zake kushika moto na kufariki papo hapo.

Mtoto wa marehemu anaitwaye Boaz Liduke (16) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya msingi Kapunga, alipoona baba yake amechelewa kurudi alimfuatilia hadi shambani alipokuwa ndipo alipomkuta baba yake amefariki nje ya kibanda cha kuhamia ndege, ndipo mtoto huyo alipochukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa uongozi wa kitongoji cha Kapunga Site one.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Kapunga Site one Bwana Ibrahimu Mwandungu ndipo alipotoa taarifa katika kituo cha polisi cha Chimala, ambapo Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuthibitisha kifo hicho kilichotokea umbali wa kilometa moja toka nyumbani kwake.

Post a Comment

 
Top