Menu
 

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jila la Bushaga Masalai mwenye umri wa mika 30, mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyabiashara kati ya Dar es Salaam na Tunduma mkoani Mbeya amefariki dunia akiwa chumba cha kupanga katika Hoteli ya High Class.

Marehemu alifika hotelini hapo Desemba 2, mwaka huu akitokea jijini Dar Es Salaam, lakini Desemba 3, wahudumu walipokuwa katika shughuli zao za usafi katika hoteli hiyo walijaribu kugonga mlango wa chumba hicho alichopanga marehemu, lakini haukufunguliwa kutokana na ukimya huo waliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi majira ya saa 6 mchana.

Hata hivyo Jeshi la polisi mji mdogo wa Tunduma baada ya kupewa taarifa lilifika hotelini majira ya saa 6 na dakika 30 ili kufanya uchunguzi na kisha kuubomboa mlango huo ndipo walipomkuta Bwana Bushanga akiwa amefariki dunia.
 
Mwili wa marehemu ulichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Tunduma ndipo Jeshi la polisi mkoa lilitoa agizo, kuwa mwili wa marehemu uhamishiwe katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya ili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuhisiana na kifo hicho kilichotokea katika mazingira ya kutatanisha.

Post a Comment

 
Top