Menu
 

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro akipokea maelezo kuhusu mikakati ya kuimarisha ulinzi na usalama mkoani hapa kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani hapa Advocate Nyombi katika kikao kilichofanyika hivi karibuni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa.
*****
Na mwandishi wetu.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja Bwana Ndangale ambaye ni Mlemavu wa viungo (60), mkazi wa kitongoji cha Igumbilo, kijiji cha Isitu  wilayani Mbarali Mkoani Mbeya anayedaiwa kumuua mwanamke (35 - 40), kisha kutoa vingo sehemu za siri Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 7 mchana, Desemba 14 mwaka huu wakati mwanamke huyo akitokea shambani, ambapo wananchi wenye hasira kali walipokuwa wakijiandaa kumuadhibu/kupokea kichapo kutoka kwa wananchi hao lakini  taarifa ziliweza kufikishwa mapema katika Kituo cha Polisi cha Chimala, na hivyo kuweza kumnusuru mlemavu huyo na kicapo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amekanusha kutokea kwa tukio hilo, lakini kulikuwepo na tukio la wanandugu kugomea kupokea maiti ya mwanamke mmoja katika Hospitali ya Chimala Mission,  ambapo madaktari walipoufanyia uchunguzi mwili huo wamesema kwamba sehemu za siri zipo salama na kisha ndugu kuchukua mwili huo na kuanza mazishi.

Ameongeza kuwa mwanamke huyo anayedaiwa kuuawa na mlemavu huyo, alikuwepo hospitalini kwa maradhi mengine.

Wakati huo huo, imeelezwa kuwa mlemavu Bwana Ndangale alishawahi kuhamishwa katika kijiji cha Mhale wilayani Mbarali kwa tuhuma za mauaji kwani inadaiwa kuwa na mtandao mkubwa wa watu wanaohusika na mauaji.

Aidha, wananchi ambao hawakupenda majina yao kutanjwa, wamemtaka mlemavu huyo kutorudi kijijini hapo kwani wamekuwa wakihofia kwenda mashambani katika msimu huu wa kilimo kwa hofu ya kuuawa na mtandao huo unaoelezewa kujihusisha na imani za kishirikina.

Post a Comment

 
Top