Menu
 

Habari na Gordon Kalulunga, Mbeya
 Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe mkoani Mbeya Bwana Thobias Mwanakatwe amevamiwa na majambazi na kuibiwa mali zake nyumbani kwake Jijini Mbeya.

 Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Mwanakatwe alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa majirani zake kuwa majambazi walikuwa wamevamia nyumbani kwake yeye akiwa safarini wilayani Kyela.

 Alisema anamshukuru Mungu yeye na familia yake hawakuwemo katika nyumba hiyo hivyo watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivunja nyumba yake na kuiba kila kitu kama hasira za kutomkuta yeye na mkewe.

Alivitaja baadhi ya vitu ambavyo watu hao waliiba ndani ya nyumba yake kuwa ni pamoja na Sub woofer mbili, Televisheni mbili,Redio aina ya Kenwood, jiko la gesi, Mtungi  wa gesi.

Vingine ni Jiko la umeme, Nguo zake zote zikiwemo suti jozi 15, nguo zote za mkewe, viatu, Magodoro, Kompyuta na vitu vingine vingi.

Post a Comment

 
Top