Menu
 

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa Advocate Nyombi ofisini kwake kuhusu mpango wa Kamati ya mafanikio ya kuimarisha Ulinzi na Usalama mkoani hapa.
*****
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka wananchi wa kata ya Garula wilayani Chunya mkoani Mbeya kuzingatia kanuni bora za afya kwa kunywa maji safi na salama ili kuepukana na na magonjwa ya milipuko hususani kipindupindu.

Kandoro ameyasema hayo hivi karibuni alipotembelea kata hiyo na kutoa pole kwa waatirika wa nyumba zao zilibomoka kwa mvua mwishoni mwa wiki ambapo alitoa msaada wa tani 47 .3 za mahindoi kwa wananchi alisema kuwa anatoa angalizo hilo kutokana na kata hiyo kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu kila mwaka .

Amesema kuwa zaidi ya watu 30 hupoteza maisha kila mwaka na hivyo ni vyema sasa wananchhi kuzingatia kanuni za afyaii kuhepukana na vifo visivyo vya lazima na kupoteza nguvu kazi kwa Taifa.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya maji yanayotumiwa na wakazi wa eneo hilo hayana usalama kutokana na maji hayo kupita sehemu nyingi hasa kipindi hiki cha mvua hivyo ni vema wananchi wakachukua tahadhari mapema ili kusiweze kutokea tatizo la vifo kama mwaka jana.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi kula matunda ambayo yameoshwa na mikono yao kunawa mara wanapotoka kujisaidia ili wasiweze kupata magonjwa ya miripuko.
Aidha kandoro alisema kuwa hii njia pekee ya kujikinga kwa kutumia njia mbalimbali ili kuweza kupambana na maradhi na kunusuru nguvu kazi kwa taifa.

Post a Comment

 
Top