Menu
 

 Utaratibu wa kujichukulia Sheria mikononi inaendelea kutawala hususan katika Mkoa wa  Mbeya. Pichani baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mwanyanje, Kata ya Igawilo  mkoani Mbeya wakiwa na nyuso za huzuni baada ya mwananchi mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja kupigwa na kisha kuchomwa moto ambao uliteketeza mwili wake. Mtu huyo alituhumiwa kuwa ni mwizi licha ya kutofahamika alichoiba au aliyeibiwa kijijini hapo.
Ukatiri usio kifani unaonekana dhahiri katika Picha hii ambapo watu wasio kuwa na huruma waliamua  kujichukulia Sheria mikononi kwa kumpiga  kisha kumchoma moto  kama inavyoonekana.
 Pichani watoto wa Kata ya Igawilo  mkoani Mbeya wakiangalia kwa  nyuso za huzuni baada ya mwananchi mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja kuchomwa moto na kuuteketeza mwili wake. Mtu huyo alituhumiwa kuwa ni mwizi licha ya kutofahamika alichoiba au aliyeibiwa kijijini hapo.
 Mwili wa Mzee Rashid Gervas (61), ukiwa katika dimbwi lililo pembeni mwa Shule ya Msingi Moto Moto Kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani mbeya.Marehemu Rashid alitoweka Nyumbani kwake Jumamosi ya Tarehe 10/12/2011 na kupatika siku iliyofuata akiwa ameaga dunia dimbwini humo.Marehemu kabla ya kifo chake alionekana katika Kilabu cha Pombe akiwa na Redio yake inayoonekana pembeni  mwa dimbwi.
Mke wa Marehemu Gervas Bi. Mwamvita Issa (52),(kushoto) akiwa na majirani zake muda mfupi baada ya mwili wa mumewe kupatikana dimbwini.

Post a Comment

 
Top