Menu
 

Habari na chanzo chetu.
Wananchi wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wamelipua lawama jeshi la polisi wilayani humo kwa kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji na kupokea rushwa kutoka kwa wananchi.

Lawama hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti kupitia barua za malalamiko ambazo zimeandikwa na wananchi na kufikishwa ofisi ya haki za binadamu.

Katika barua hizo wananchi wamelilalamikia jeshi hilo kwa kubambikizia wananchi kesi, baadhi ya viongozi wa vituo vya polisi kutishia kuuwa raia wanapofatilia haki zao na kushiriki kuwanyima haki wakulima pindi wanapokuwa kwenye migogoro na matajiri.

Aidha wananchi hao wamemuomba kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi kuwachukulia hatua za kisheria askari wake ambao wamekuwa wakitumia nafasi ya uaskari kunyanyasa raia.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi ameahidi kufuatilia malalamiko hayo na kuwataka wananchi kufikisha malalamiko kwenye ofisini yake badala kufikisha taarifa kwa watu ambao hawataweza kudhibiri tabia hizo

Post a Comment

 
Top