Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Rungwe.
Watu wawili jinsi ya kiume wamekutwa wameuawa na wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Kinyika, kata ya Ikuti wilaya ya Rungwe wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya wizi.

Watu hao wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya marehemu kufanikiwa kuvunja kisha kuiba vitu mbalimbali vya thamani kwenye nyumba ya bwana Zakayo Ngela ambapo mara baada ya marehemu hao kutenda tukio hilo bwana Zakayo alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa wananchi ambao walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa hai.


Hata hivyo uhai wa watuhumiwa hao ulikatishwa na wananchi wenye hasira kali ambao walikuwa wakiwashambulia wezi hao kwa kutumia vitu mbalimbali vigumu.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa upelelezi zaidi unaendelea wa tukio hilo na kuwataka wananchi kuwafikisha watuhumiwa kwenye vituo vya polisi badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Post a Comment

 
Top