Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Watu wawili wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio mawili tofauti, likiwemo la mtoto wa kiume anayejulikana kwa jina la Juhudi Stephano mwenye umri wa miaka mitatu na nusu ambaye amefariki baada ya kutumbukia katika kisima kinacho chibwa na baba yake katika kijiji cha Kasale Idiga Kata ya Bonde la Songwe wilaya ya Mbeya vijijini.

Tukio hilo limetokea majira ya mchana ambapo marehemu alitumbukia katika kisima hicho, ndipo baba yake Bwana Stephano Julius alipogundua kutumbukia kwa mwanae na kisha kutoa taarifa kwa Afisa mtendaji wa kijiji Bwana Marko Mwaigaga ambaye naye alitoa taarifa Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.

 Baada ya uchunguzi kufanywa na Jeshi la Polisi mwili wa mtoto Juhudu ulikabidhiwa kwa wanandugu ili kuwapa fursa ya kufanya mazishi.

Tukio lingine katika kitongoji cha Maporomoko katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Nick na anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kile kinachodaiwa na wananchi hao kuwa marehemu amekuwa akijihusisha na vitendo vya Ujambazi.

Marehemu alipingwa na wananchi wasiofahamika na kupa kichapo hadi mauti yalipomfika majira ya saa tatu usiku Desemba 13, mwaka huu.

Diwani wa Kata ya Tunduma Bwana Frank Mwakajoka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwani wahalifu wanapokamatwa wapeleke kwenye vyombo vya sheria ili kuweza kuchukua mkondo wake.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio yote mawili na kwamba wananchi wanatakiwa kuwa waangalifu kwa watoto na kuwaweka mbalina visima vya maji ili kuepesha vifo, pia ameendelea kutoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata watuhumiwa.

Post a Comment

 
Top