Menu
 


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, akizungumza na vyombo vya habari nchini.
*******
 Habari na Mwandishi wetu
Mfanyabiashara maarufu Jijini Mbeya Changa Konzo mkazi wa eneo la Soweto mtaa wa Block Q Jijini Mbeya anashilikiwa na Jeshi la polisi mkoani hapa kwa kosa la kumbaka mwanae wa kumzaa.

Konzo alimtendea kitendo hicho mwanae huyo (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka (12) nyumbani kwake majira ya saa tano usiku baada ya purukushani nzito kati ya Baba huyo na binti yake mkubwa.

Taarifa za uchunguzi zilizothibitishwa na familia ya mfanyabiashara huyo wakiwemo wanaharakati wa kutetea haki za unyanyasaji wa Jinsia Jijini hapa zimesema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 8 mwaka huu.

Baadhi ya wanafamilia wa mfanyabiashara huyo wakiwemo watoto wake ambao ni mashuhuda, walisema kuwa jaribio la kwanza la mfanyabiashara huyo liliaza majira ya saa Nne usiku na huku Baba huyo akimuoba binti yake mkubwa alale chumbani kwake.

''Alituomba sisi mabinti zake tulale nae chumbani kwake na kusema kuwa tungefanya hivyo angepona ugonjwa wake unaomsumbua wa kutozaa watoto wengine na kwamba tutaishi maisha mazuri zaidi jambo ambalo tulikataa kisha akaaza kumvuta mmoja wetu'' alisema shuhuda huyo.

Alisema baada a kuanza kumvuta binti huyo aliyembaka akashindwa nguvu na binti yake mkubwa na hatimaye binti huyo mkubwa alimuomba ambake yeye lakini alikataa na hatmaye akatumia njia zingine na kumchukua binti aliyembaka na kumwingiza chumbani kwake na kumfanyia tendo hilo.

Mashuhuda hao walisema kuwa baada ya Baba huyo kutimiza adhima yake, mtoto huyo alilia jambo ambalolilimshtua dada yake ambaye aliamka na kwenda chumbani kwa baba yake ambako alipewa Shilingi Elfu kumi na akatoka na mdogo wake nje ya nyuma majira ya saa nane usiku.

''Tulipotoka nje ya nyumba huku mdogo wangu akiw amejifunika shuka, ndipo mdogo wangu mwingine wa kiume akaja na kuniambia kuwa Baba amemwamuru avue nguo alale uchini ndipo tukaondoka'' alisema mtoto wa mfanyabiashara huyo.

Alisema suala hilo ni la pili baada ya kushindwa jaribio lake la kwanza kwake ambapo watoto hao tangu Novemba 2, 2011 wanaishi na Baba yao huyo baada ya Mama yao kuwa kwa wazazi wake baada ya kuumizwa kwa kipigo na mumewe.

Wanaeleza zaidi kuwa baada a hayo yote waliomba hifadhi kwa majirani na hatimaye wakatoa taarifa katika kituo kidogo cha Mwanjelwa na kisha wakaenda kumtibu mtoto huyo katika Hospitali ya wazazi Meta ambako mtoto alikutwa na michubuko huku shahhawa zikiwa zimeganda katika mapaja yake.

Baada ya hapo walirudi Polisi na hatimaye Kamanda wa polisi wa wilaya ya Mbeya Silvester Ibrahim akatoa amri ya mtuhumiwa kukamatwa January 9 mwaka uu majira ya saa mbili usiku.

Akizungumzia suala hilo, Mratibu wa kitengo cha msaada wa sheria Jijini Mbeya (MBEPAU) Jane Lawa, alisema kuwa suala hilo limewafikia na wanafanya utaratibu wa kulishughulikia kwa ajil ya kupinga ukatili huo wa kijinsia.

Alisema kuwa katika Jiji la Mbeya ukatili wa namna hiyo huku baadhi ukihusishwa na masuala ya ushirikina wa kupata utajiri, yamekuwa mengi lakini masuala hayo yanashindwa kudhbitiwa kutokana na udhaifu wa baadhi ya watendaji wa vyombo vinavyosimamia sheria.

Post a Comment

Mdau USA said... 19 January 2012 at 06:49

YAANI NINA SHIKWA NA HASIRA MPAKA BASI NA HALI HII YA UKATILI. SASA HII CASE SI IKO WAZI TU KWANINI HUYU MZEE ASIPELEKWE MAHAKANI JAMANI? KAMA KAATHIRIKA SI NDIO KAMUUA KABISA MTOTO WAKE, HUU NI UKATILI ULIOKITHIRI KWA KWELI. NAOMBA UTUJULISHE HATMA YA HUYU MZEE TFADHALI

 
Top