Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Gari ya Kampuni ya Ulinzi binafsi ya G4S iliyokuwa ikitokea mji mdogo wa Tunduma, wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya imekamatwa na Mamlaka ya mapato nchini (TRA) Mkoa wa Mbeya, ikiwa na bidhaa haramu(vipodozi).

Tukio hili limetokea Januari 6, mwaka huu gari hilo lililofukuziwa na Maafisa wa doria kutoka TRA na kisha kulikamatia eneo la Songwe, wilaya ya Mbeya vijijini na kuvikamata vipondozi hivyo na wanawake wawili ambao ni wamiliki wa vipodozi na Askari wa wawili wa Jeshi la Polisi na Askali wengine wa Kampuni hiyo ya ulinzi.

Mtandao huu umeshuhudia gari hilo lenye nambari za usajili T.690 AMA aina ya Toyota Landcruiser likiwa katika uzio wa Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA), mkoa wa Mbeya.

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoani hapa Bwana Anord Maimu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo licha ya kuwa nje ya ofisi kikazi na kwamba suala hilo ameliachia Jeshi la Polisi mkoani hapa.

Wakati huohuo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amekiri kupokea taarifa hizo kutoka kwa Meneja wa TRA mkoani hapa na kwamba Askari wake waliohusika na usafirishaji wa bidhaa hizo haramu wakibainika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kijeshi.

Bwana Maimu amesema Mamlaka ya mapato nchini kwa mkoa wa Mbeya imeteketeza vipodozi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 129, vilivyokamatwa kwa kipindi cha mwaka uliopita.

Ametoa onyo kwa wananchi wanaojihusisha na biashara hiyo haramu kuacha mara moja, kutokana na utumiaji wa vipodozi hivyo kuathiri afya hali ambayo husababisha ugonjwa wa Kansa.

Post a Comment

 
Top