Menu
 

Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dokta Seif Mhina, akizungumza na madaktari wa Hospitali na Zahanati binafsi katika Ukumbi wa Youth Centre uliopo katika Jiji la Mbeya.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Hospitali binafsi zilizopo mkoani Mbeya zimeaswa kutotumia dawa za Serikali katika zahanati na hospitali ili kuepuka kufungiwa.

Hayo yamesemwa na Dokta Reinfredy Chombo wakati akitoa maada katika ukumbi wa youth centre jijini mbeya alipokutana na wamiliki wa hospitali hizo mwishoni mwa juma.

Chombo amesema katika ukaguzi kuna baadhi ya zahanati zimekutwa zikitoa dawa zilizoidhinishwa kwa matumizi ya hospitali za serikali hivyo kusababisha upungufu wa dawa katika hospitali hizo,na kuongeza kuwa kuna baadhi ya wahudumu katika hospitali hizo hawana vyeti na hivyo kufanya maisha ya wananchi kuwa mashakani.

Aidha Chombo amesema vituo vingi hapa mkoani havitumii kanuni za usafi na hivyo kuhatarisha afya za wagonjwa na kwamba wawe na tabia ya kujikagua wenyewe kabla ya kukaguliwa pia kutumia vifaa sahihi katika utabibu kwani kuna baadhi ya vituo vimekuwa vikitumiwa kutolea mimba hiyo ni kinyume na sheria ya nchi.

Post a Comment

 
Top