Menu
 

Habari na Mtandao huu
.Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Emmanuel Kyando anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 45 hadi 50 mkazi wa Mbeya, amefariki dunia mkoani Mbeya baada yawananchi wenye hasira kali kumkamata na kupiga na kisha kumchoma moto.

Tukio hili limetokea katika kijiji cha Mbugani wilaya ya Chunya usiku wa kuamkia Desemba 31, mwaka 2011 wakati marehemu akijaribu kuiba katika maduka mawili ya wakazi wa kijiji hicho yanayomilikiwa na Asomwisye Mwaijumba na Shukrani Inyasi.

Mara baada ya wananchi hao wenye hasira kali kuuchoma moto mwili huo walitawanyika n akuacha mwili wa marehemu kandokando ya barabara ambapo mwili wake uligunduliwa na baadhi ya wananchi waliokuwa wanaenda shambani hivyo kutoa taarifa kwa Afisa mtendaji wa kijiji Bwana Emmanuel Evance ambaye naye alitoa taarifa katika Kituo cha polisi wilaya ya Chunya.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa onyo kwa wananachi kutojichukulia sheria mkononi na kwamba mhalifu akikamatwa apelekwe kwenye mikono ya sheria ili sheria iweze kuchukua mkondo wake, badala ya kuhukumu wananchi wenyewe.

Hata hivyo ameongeza kuwa  Jeshi la polisni litawakamata na kuwachukulia sheria wale wote watakaojihusisha na mauaji kwa kisingizio cha wananchi wenye hasira kali.

Post a Comment

 
Top