Menu
 

Habari na mwandishi wetu.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Jamesi mwenye umri wa miaka 40 amenusurika kifo baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16 makazi wa kata ya Ilemi jijini Mbeya.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili za asubuhi ambapo mtuhumiwa huyo aliingia nyumbani anakoishi binti huyo wakati akiwa peke yake na kuanza kumuingilia kimwili bila ridhaa ya mwanamke huyo.

Wakazi wa eneo hilo walipata taarifa ya kubakwa kwa binti huyo baada ya kusikia kelele zikitoka ndani ya nyumba na kwamba baada ya kufika walimkuta kijana huyo akimwingia kimwili binti huyo ambaye tumemuhifadhi jina kwa sababua za kimaadili.

Mama mzazi wa mtoto huyo amesema kuwa mwanae ameingiliwa kimwili na kijana huyo wakati yeye akiwa katika biashara zake ndogondogo.

Kwa upande wake balozi wa mtaa huo wa Ilemi darajani Khamadi Mwakajinga amesema pamoja na mtuhumiwa kukamatwa wananchi waliafikiana kumwachia kijana huyo kutokana na kile alichokieleza kuwa mtuhumiwa ametoa gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais.
 
Mtandao huu unahoji ni kwanini viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia sheria, wakishindwa kusimamia kutoka gerezani sio sababu ya kuendelea kufanya uhalifu tena.

Post a Comment

 
Top