Menu
 
Mfugaji Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser  lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo. 
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mgogoro kati ya wakulima, wanakijiji na mwekezaji wa shamba la Kapunga kampuni ya Export Traders lililopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya huenda ukawa endelevu kutokana na Serikali kushindwa kutolea ufafanuzi hatma ya mgogoro huo ambao umekuwa ukiwasababishia wanakijiji wa Kapunga kujeruhiwa na kukosa haki zao za msingi.

Utata wa kumalizika kwa mgogoro huo umetokana na Waziri wa kilimo na Chakula ushirika Profesa Jumanne Maghembe kushindwa kuzungumza lolote pindi alipoombwa na waandishi wa habari kuzungumzia hatma ya mgogoro huo.

Wanahabari walilazimika kumtaka Waziri Maghembe kuzungumzia suala hilo baada ya kutoa kauli katika kikao cha wakulima wa zao la kahawa na viongozi wa Serikali mkoani Mbeya kuwa viongozi wanatakiwa kusimamia vyema bei za mazao badala ya kuwaachia walanguzi wakiendelea kuwanyonya wakulima.

Hivi karibuni Mwekezaji wa Kapunga Rice Project amekuwa akiwanyanyasa wakulima wa zao la mpunga kwa kuwapiga viboko, kuwasababishia majeraha mbalimbali kwa kuwagonga na gari ikiwa ni pamoja na kuuwa mifugo yao huku mwekezaji huyo akiachwa bila ya kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

Post a Comment

 
Top