Menu
 

Katikati mwenye koti jeusi diwani wa kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka Baada ya wafanyabiashara kushindwa kufanyabiashara zao na kupelekea kufunga kutokana na vurugu zilizotokea za kupingwa ucheleweshaji wa matokea ya uchaguzi nchini Zambia sasa ni shwari na wananchi wameanza kuvuka mpaka na wafanyabiashara kurejea katika shughuli zao.
 
Madereva wakielekea kukamilisha ushuru wa forodha na kukamilisha taratibu za kuvuka mpaka kuelekea nchini Zambia na Kongo. (Picha kutoka Maktaba yetu)
 *****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Siku ya tatu mfululizo madereva wa magari ya mizigo wameendelea kugoma katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Mbeya, kutokana na waajiri wao kutofanyia kazi madai yao.

Baadhi ya madai ya madereva hao ni pamoja na kulipwa mishahara midogo, kunyimwa pesa za kujikimu safarini, kutokuwa na makato ya mafao ya uzeeni.

Madereva hao wameamuka kutovuka mpaka pia kuingia nchini kwa madai ya kupatiwa ajira ya kudumu na waajiri wao suala ambalo liliingiliwa kati na Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu mwishoni mwa mwaka jana, jambo ambalo waziri huyo aliahidi kulitatua suala hilo

Kutokana na msongamano wa magari hayo kumepelekea shughuli za kiuchumi kudhorota katika mji wa Tunduma kwani wengi wamekuwa wakitegemea wageni kutoka nchi za kusini mwa Afrika kama vile Congo, Botswana, Zimbabwe, Lesotho, Namibia na Afrika Kusini ambao wengi hutegemea mpaka wa Tunduma kupitishia bidhaa zao.

Mbali na usumbufu huo Diwani wa mji mdogo wa Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka amesema ajali nyingi zimekuwa zikitokea kutokana na msongamano huo, pia wakazi wengi wamelazimika kutembea kwa miguu kutokana na magari kushindwa kupita katika barabara ya Tunduma/Sumbawanga na Tunduma/Mbeya.

Aidha Mwakajoka amesema uchafuzi wa mazingira umekuwa ukifanywa na madereva hao kutokana na kukosa pesa za matumizi hivyo kukosa malazi hali inayowalazimu kujisitiri chini ya uvungu wa magari.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gilbert Kimoro amesema wamechukua tahadhari ya kuandaa gari la wagonjwa kutokana na hofu ya mlipuko wa magonjwa, ili kukabiliana na lolote linaloweza kutokea .

Wakati huo huo Kimoro amesema kuwekuwa na hofu ya usalama kutokana na madereva hao kutosafiri na muda mwingi kuwepo mahali pamoja hali inayoweza kuleta uvunjifu wa amani, pia amebainisha hivi sasa madereva wameanza kujaza fomu zilizotolewa na SUMATRA, ingawa madereva hao wamesema pamoja na kujaza fomu hizo hawataweza kuendelea na safari.

Amesema suala hilo limecheleweshwa na madereva hao kutokana na mchakato wa katiba wa madereva hao ambao ulianza mwaka uliopita.

Ili kuhakikisha amani inakuwepo Tunduma, Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amepiga kambi mpakani hapo kwa siku mbili mfululizo ili kuhakikisha amani na utulivu mpakani pia kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Post a Comment

 
Top