Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Bi Rahabu Robert (26) mkazi wa mtaa wa Manga A, jijini Mbeya amekutwa amemfunga kamba ya katani kwenye meza mtoto wake wa kumzaa aitwaye Eliza Frank (4), kwa kile alichodai kuchoshwa na tabia mbaya ya uzurulaji.

Tukio hilo limetokea Januari 25, mwaka huu nyumbani hapo majira ya saa 10 jioni na mtoto huyo kukutwa majira ya saa 12 jioni na majirani wakati mama huyo akiwa kanisani kwenye ibada.

Baada ya majirani kubaini ukatili huo walimtaarifu Mwenyekiti wa mtaa Bi Rose Mwaisanga, ambapo naye alimfuata mama huyo kanisani katika Kanisa la Moravian Ruanda lililopo karibu na Hospitali ya K'S lililopo mtaa wa Mafiati.

Wakati huo huo baada ya kufika nyumbani mama huyo na mwenyekiti walimkuta mtoto huyo akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali ya kamba hiyo, na kulazimika kumfungua mtoto na mama wa mtoto huyo kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati.

Mwenyekiti wa mtaa huo Bi Rose na mwandishi wa mtandao huu walikuwa na wakati mgumu wa kumnusuru mama huyu asipigwe na wananchi wenye hasira kali, kutokana na kumpiga mama huyo pasipo kujali mtoto mchanga aliyembeba mgongoni na kuingizwa kwenye daladala hali ambayo ilisababisha wananchi hao kuipiga mawe daladala hiyo wakidai mama huyo naye aadhibiwe.

Kwa upande wake Baba mzazi wa mtoto huyo Bwana Frank Anangisye (29), amesema kuwa alikuwa hana taarifa yoyote juu ya mateso ya mwanae na kuwashukuru majirani kwa kuweza kufichua uovu wa mkewe.

Hata hivyo mama wa mtoto huyo Bi Rahabu anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa Jeshi la polisi kukamilika. 

Post a Comment

Ngeze....(Nesha) said... 26 January 2012 at 12:13

Kwan huko Mbeya kuna matatizo gan jamani?,mbona watu wakatili sana?!.

Chimbuko Letu said... 29 January 2012 at 13:14

Kila kukicha Mbeya mpya jamani yaani matukio kutwa nzima @ Nesha

 
Top