Menu
 

Habari na Mtandao huu, Mbeya.
Robert John Hasani mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Majengo jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la ubakaji.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Monika Ndyekobora mwanasheria wa Serikali Fransisi Rojasi amesema disemba 25 mwaka jana mshatakiwa alimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 36 kinyume na kifungu cha sheria namba 130 B na kifungo 131 sura ya kwanza ya marekebisho ya mwaka 2002.

Mstakakiwa amerudishwa rumande kwa kutokidhi masherti ya dhamana ambapo dhamana ni shilingi milioni mbili na kwamba kesi hiyo itasomwa tena Februari pili mwaka huu.

Siku hiyo hiyo Eva Mwakibinga mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Makunguru amefikishwa katika mahakama hiyo ya mkoa kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi wifi yake.

Mwanasheria wa Serikali Fransisi Rojasi amesema mshtakiwa ametenda kosa hilo la kumpiga, kumng'ata Fransiska Ediani na kumsababishia maumivu shavu lake la kushoto kinyume na kifungo cha sheria namba 225 sura ya 16, hata hivyo hakimu Monika Ndyekobora ameihairisha na huku ya kesi hiyo itatolewa Februari pili baada ya mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo.

Post a Comment

 
Top