Menu
 


Habari na Mwandishi wetu
Neema Edson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Namtanga Swaya jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kumuua mtoto wake akiwa mchanga.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawizi Monika Ndyekobola mwanasheria wa serikari Ema Msofe amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 3 mwaka huu maeneo ya namtanga jijini hapa.

Amemtaja mtoto aliyeuawa kuwa Steven Chinga ambaye alikuwa na umri chini ya miezi kumi na miwili kinyume na kifungu cha sheria namba 199 sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na dhamana ya kusikiliza kesi kama hizo na kesi hiyo itaanza kusomwa upya februari 6 mwaka huu katika mahakama kuu.

Post a Comment

 
Top