Menu
 
Mfugaji Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser  lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo. 
*****
Habari na Mwandishi wetu, Mbarali
Wananachi wa kijiji cha Kapunga wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameingiwa na hofu ya maisha yao baada ya mwekezaji wa shamba la Kapunga kampuni ya Export Trading kumwaga viwatilifu ambavyo vinadhaniwa kuwa na sumu karibu na mashamba yao.

Wananchi hao wamesema kuwa viwatilifu hivyo vimeunguza mpunga na kusababisha mazao mbalimbali kuungua katika mashamba yao.

Mkuu wa wilaya ya Mbarali Kanali Kosimasi Kayombo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi tayari umeshaanza na ametuma timu ya wataalamu kutoka idara ya kilimo na ardhi kikiwa chini ya kamanda wa polisi wilaya ya Mbarali.

Post a Comment

 
Top