Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Afisa mtendaji kata ya Iyela bwana Ezekiel Kipako amesema ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya Sekondari Iyela umechelewa kutokana na uhaba wa fedha pamoja na vitendea kazi.

Amesema kamati ya ujenzi wa shule ya Sekondari Iyela ulipanga kukusanya shilingi milioni Ishirini na nane na laki tatu lakini hadi sasa wamekusanya shilingi milioni sita laki saba sitini na mbili elfu na mia nane.

Bwana Kipako ameongeza kuwa fedha hizo zingeweza kutosheleza kujenga vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi 500 waliochanguliwa kujiunga na shule ambapo hadi sasa ni wanafunzi 200 ndio wameanza masomo yao ya sekondari kati ya hao 500.

Wakati huohuo amesema kuwa mtaa wa Block T ulipangiwa kukusanya shilingi milioni mbili laki tatu na sababini elfu lakini imekusanya shilingi laki nane arobaini tisa elfu, mtaa wa Nyibuko ulipangiwa shilingi milioni mbili laki saba na elfu hamsini lakini imekusanya shilingi laki saba na arobaini na sita elfu.

Hata hivyo amesema kuwa mtaa wa Mapambano licha ya kushindwa kufikia malengo yake ya kukusanya mchango wa shilingi milioni nne laki moja na elfu hamsini lakini wamekusanya shilingi milioni moja na elfu sitini na mbili.

Post a Comment

 
Top