Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Watu sita wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa Mbeya kwa tuhuma za wizi  wa tumbaku Oktoba 22, mwaka uliopita maeneo a Songwe wilaya ya Mbeya vijijini.

Akisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi Monika Ndyekobola  mwanasheria wa serikali Faraja Msuya amesema washitakiwa wote sita waliiba magunia 123 ya tumbaku  kinyume na kifungu cha sheria namba 265 na 269 marekebisho ya mwaka 2002.

Amewataja washitakiwa  hao kuwa ni Marijan Rajabu mwenye umri wa miaka 24, Mhima Shaban mwenye umri wa miaka 26 Innocent Mwalwanda mwenye umri wa miaka 30, Shaban Mshana mwenye umri wa miaka 37, Leonard Mgaya mwenye umri wa miaka  26 na Peter Kiwelo.

Hata hivyo washtakiwa wote walikana shtaka na kwamba kati ya washtakiwa hao washtakiwa sita wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni nane huku mmoja kati yao akirejeshwa rumande baada ya kukosa dhamana.

Kesi hiyo itasomwa tena January 24 mwaka huu.    

Post a Comment

 
Top