Menu
 

Wimbi la ajali ya magari ya mizigo/maroli mkoani Mbeya lazidi kutanda, kutokana na madereva kutochukua tahadhari ya mwendokasi, licha ya mvua zinazoendelea kunyesha katika msimu huu wa masika. Pichani Askari wa Kikosi cha Usalama wa barabarani akifanya uchunguzi wa ajali ya tela la roli lenye nambari ya usajili T  563 AAH na kichwa cha roli aina ya Scania yenye nambari T 504 ARA, lililokuwa likiendeshwa na dereva Juma Mombeki kutoka Jijini Mbeya kuelekea Jijini Dar es salaam na kisha kupinduka Mlimanyoka jijini Mbeya.
Tela la roli lenye nambari ya usajili T  563 AAH na kichwa cha roli aina ya Scania yenye nambari T 504 ARA, lililokuwa likiendeshwa na dereva Juma Mombeki kutoka Jijini Mbeya kuelekea Jijini Dar es salaam na kisha kupinduka Mlimanyoka jijini Mbeya.

Kupishana kwa magari ya mizigo ndio sababu ya kupinduka kwa tela la roli lenye nambari ya usajili T  563 AAH na kichwa cha roli aina ya Scania yenye nambari T 504 ARA, lililokuwa likiendeshwa na dereva Juma Mombeki kutoka Jijini Mbeya kuelekea Jijini Dar es salaam katika eneo la Mlimanyoka kama inavyoonesha pichani, roli hilo likipishan ana roli jingine lenye nambari T 620 AUU lenye tela nambari T 468 AZH lililokuwa likielekea nchi ya Zambia kutokea Jijini Dar es salaam.
Msongamano wa magari eneo la Mafiati jijini Mbeya bado halijafanyiwa ufumbuzi, ikiwa ni pamoja na kuweka taa za barabarani, licha ya kuwepo kwa ajali za mara kwa mara hasa mida ya jioni. (Picha na Chimbuko Letu.)

Post a Comment

 
Top