Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wimbi la ubakaji mkoani Mbeya limeendelea kushika kasi baada ya Mzee mwingine aliyefahamika kwa jina la Frank Mwakyeja (60 - 65), mkazi wa mtaa wa Ilolo B kata ya Isanga jijini Mbeya kuwabaka watoto wawili wa rika tofauti.

Tukio hilo limetokea Desemba 5, mwaka uliopita ambapo aliwabaka watoto hao wa jirani yake mmoja akiwa mwanafunzi wa Shule ya msingi Manga, jijini hapa mwenye umri wa miaka 9 na mwingine mwanafunzi wa shule ya msingi Madaraka jijini hapa mwenye umri wa miaka 7 (majina yao yanahifadhiwa).

Akizungumza na Mtandao huu Baba wa mmoja wa watoto walitendewa ukatili huo Bwana Gwakisa Mwakihaba (38), alifungua jarada la mashitaka MWJ/RB/270/2011, mnamo Desemba 6, mwaka jana na baadae jarada hilo kuhamishiwa Kituo kikuu cha Kati na kufunguliwa jarala namba MB/IR/10539/2011, ambapo mtuhumiwa alikamatwa na kuachiwa hali ambayo inapelekea hasira kwa wananchi iweje mtuhumiwa huyo aachiwe pasipo sababu maalumu.

Hata hivyo kwa mujibu wa wananchi hao waliokuwa na manung'uniko wamesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwabaka watoto 6. mtaani hapo wakiwemo watoto mapacha, ambapo vitendo hivyo vimetafsiriwa kuwa nivya imani za kishirikina, hali ambayo ilipelekea wake wa mtuhumiwa huyo kukimbilia kwao mkoani Morogoro na mwingine Jijini Dar es salaam, kutokana na kuchoshwa na vitendo hivyo vya ubakaji vinavyotendwa na mume wao.

Watoto hao kwa pamoja wamefanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Wazazi ya Meta, Desema 6 na 7 mwaka uliopita na Daktari kubaini kuwa watoto hao walibainika kuingiliwa kimwili.

Kwa upande wake Bibi wa watoto hao Bi Ezelina Mwakihaba (70), amesikitishwa na kitendo cha mmoja wa wapelelezi wa kesi hiyo kuchelewesha uchunguzi na kutaka wafanye mazungumzo. licha ya familia ya mtuhumiwa kudai kutoa vitisho vya mauaji kwa hiyo.

Post a Comment

 
Top