Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
John Jackson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Mbeya Pick amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 maeneo ya Mbeya Pick.

Akisoma shtaka hilo mwanasheria wa Serikali Faraja Msuya mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Monica Ndyekobora amesema mshtakiwa alimbaka mtoto huyo disemba 21 mwaka jana katika maeneo ya Mbeya Pick.

Amesema kuwa kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha Sheria namba 130 kifungu cha pili E na kifungu cha 131 sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi January 31 mwaka huu na mtuhumiwa amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
 
Wakati huohuo Fransis Anyosisye Mwakatika mkazi wa Soko matola jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya hakimu makazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la mauaji eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini.

Akisoma shtaka hilo Mwanasheria wa Serikali Adolfu Maganda mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Kusaga Majinge amesema kuwa mshtakiwa Fransis Mwakatika alimuuwa Fred Manji mwezi disemba mwaka jana.

Kitendo hicho ni kinyume cha Sheria kifungu namba 196 sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujieleza chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na dhamana ya kusikiliza kesi hiyo, na kwamba mahakama kuu pekee ndiyo yenye dhamana ya kusikiliza kesi hiyo.

Post a Comment

 
Top