Menu
 


Habari na Mwandishi wetu.
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani Mbeya aligongwa na moja ya mgari yaliyokuwa kwenye msafara wa Ziara ya siku tatu ya Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal mkoani hapa.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na mbili jioni  Februari 25 mwaka huu wakati msafara wa magari wa kutokea Wilaya ya Mbarali kuelekea Jijini Mbeya.

Majeruhi alifahamika kwa jina la Franu Elia (28) ambapo aligongwa na gari hilo wakati akiendesha baiskeri  wakati msafara huo ulipokuwa unapita.

Pia Franu  aliokotwa na msamalia mwema Faines Mwalemba , Agnes  Kahawa  ambao waliomba msaada katika gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 247  BFL lililokuwa likiendeshwa na Bwana John Mgaya  na msaidizi wake Justin Milaji ambao walimpeleka katika kituo cha polisi  cha  Inyala  na kupewa PF3 na kisha kuelekea Kituo cha afya  cha Inyala.
 
Hata hivyo kutokana na kujeruhiwa vibaya sehemu ya kichwani hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi, wauguzi wa kituo cha afya Inyala walimtaka mgonjwa kupelekwe hospitali ya RUFAA jijini Mbeya, ambapo amelazwa mpaka sasa.

Lakini jitihada za kumtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Advocate Nyombi ali aweze kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo  ziligonga mwamba kutokana na Kamanda huyo kuwa katika msafara huo.

Post a Comment

 
Top