Menu
 

Habari na mwandishi wetu.
Shida Sasumba (37) mkazi wa Sinde jijini Mbeya amekunywa sumu na hali iliyompelekea kufikwa na mauti, baada ya kupoteza shilingi elfu kumi na tatu.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao hawakupenda majina yao kutajwa wamesema wakati wanapitisha michango kwa wakazi wa mtaa huo kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu Shida kuelekea katika wilaya ya Kyela mkoni Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Jakobu Mwalyepere amesema kuwa marehemu alikunywa sumu Februari 26 mwaka huu, na badaye alichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha polisi cha Kati kilichopo jijini hapa ambapo alipewa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya.

Aidha Mwalyepele aliongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa mkoni Mbeya kwa ajili ya kusubilia taratibu za kusafilisha mwili huo kuelekea katika wilaya ya kyela mkoni hapa.

Pia taaRIfa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa na mtoto mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Hawa Sasumba ambaye alikuwa akiishi naye katika mtaa huo.

 Hata Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya  Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hosipitali ya Rufaa mkoani hapa.

Post a Comment

TANZANIA said... 29 February 2012 at 03:42

mmmmmmmmmmmmmmmmh hiyi hataree!

Chimbuko Letu said... 29 February 2012 at 03:53

Jamani ugumu huu wa maisha sijui tusaidiane kivipi? wanajamii

Anonymous said... 29 February 2012 at 08:23

Kwel kuna wa2 wanamaisha magumu ona sasa pesa yake mwenyewe leo inamuingiza kaburini

 
Top