Menu
 


Habari na Mwandishi wetu.
Kanisa la Free Pentecostal Of Tanzania limeanza mchakato wa uanzishwaji wa baraza la watoto wenye ulemavu Mkoani Mbeya ikiwa ni utekelezaji wa ombi la watoto hao, walilolitoa katika sherehe za uzinduzi wa Sera ya kanisa hilo kuhusu ulemavu zilizofanyika Jijini Dar es Salaam mwaka 2008.

Mchakato huo umeanza kwa kanisa hilo kufanya kikao cha wadau wa maswala ya mtoto na ulemavu mkoani hapa ikiwashirikisha Maafisa Elimu, Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii pamoja na Wakurugenzi kutoka Halmashauri zote za Mkoa huu.

Mratibu wa uanzishaji wa baraza hilo, Lucas Mhenga amesema kuwa katika kufikia malengo hayo kanisa lilichukua hatua ya awali kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kupata mawazo ya namna ya kuanzisha na kuendesha baraza hilo.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ambaye ni Katibu Tawala msaidizi, Mipango na Utawala Mkoa, Nicolaus Mtambi amesema Serikali inaunga mkono juhudi za kanisa hilo za kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha azma ya serikali na kanisa ya kuwekeza kwa watoto kwa mstakabali wa Taifa la kesho.

Post a Comment

 
Top