Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Chama cha maalbino Mkoa wa Mbeya kinawaomba wahisani mbalimbali wakiwemo wananchi wa kawaida kuwapatia msaada wa fedha kwa ajili ya semina elekezi na mikutano ya hadhara.

Ombi hilo limetolewa na katibu wa chama hicho Williamu Simwali wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kuhusu vikwazo vya maendeleo ya chama cha maalbino mkoani Mbeya kwa mwaka 2011.

Simwali amesema zaidi ya shilingi Milioni 35 zinahitajika kwa ajili ya kuendesha semina elekezi kwa wanachama pamoja na mikutano ya hadhara kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi jinsi ya kuishi na maalbino. 

Amesema kiasi hicho cha fedha kitasaidia kufanya ziara wilayani ya kuwatembelea wanachama ambao ni maalbino ili kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo. 

Wakati huohuo amesema mkoa wa Mbeya unajumla ya maalbino 263.

Post a Comment

 
Top