Menu
 

 Licha ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, kuzuia magari ya mizigo maarufu kama Malori kubeba abiria, hali imekuwa tete kutokana na Askari wa usalama wa barabarani Kituo cha Mlowo, barabara ya Mlowo/Kamsamba wamekuwa wakiruhusu magari hayo kupakia abiria kupita kiasi kama inavyoonekana pichani. Mbali na askari hao kufanya ukaguzi hali hii imekuwa ikifanyika kila siku majira ya asubuhi na mchana. 
Mtandao huu umeshuhudia gari hii ya mizigo ikiwa imebeba abiria na mizigo kama baiskeli, vinywaji ikiondoka kutoka Mlowo kuelekea Kamsamba wilaya ya Mbozi, licha ya kukaguliwa na Askari wa usalama wa barabarani na kuruhusiwa kuondoka, ambapo kwa hali hii inatishia usalama wa abiria. (Picha zote na Ezekiel Kamanga, Mbozi).

Post a Comment

 
Top