Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Isanga wameulalamikia utawala wa shule hiyo kutoza michango mbalimbali.

Malalamiko hayo yametolewa katika kikao cha waalimu na wazazi kilichofanyika hivi karibuni shuleni hapo kikiwa na le lengo kujadili ongezeko la matumizi ya shule hiyo.

Miongoni mwa vitu vilivyolalamikiwa ni gharama ya maji ambayo imepanda kutoka shilingi elfu tatu mia sita hadi elfu nne, michango ya masomo ya ziada, michango ya ndoo za maji, hela ya kuchapishia mitihani ambapo kwa mwezi mzazi mmoja huchangia shilingi elfu kumi na tatu na mia tano.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Hasimu Kanjoka amesema suala la michango lilianza tangu awali na kwamba wazazi ndio wenye uwamuzi wa kuwepo kwa michango hiyo.

Hivi karibuni naibu waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi Filipo Mulugo alitoa agizo kwa maafisa elimu nchini kutoa adhabu kwa waalimu ambao watabainika kukusanya michango kutokana na kile alichokieleza kuwa Serikali haiitambui michango hiyo.

Post a Comment

 
Top