Menu
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya uchimbaji Makaa ya Mawe, Tancoal, Graeme Robertson, wakati alipotembelea mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe unaoendelea eneo la Ruanda Wilaya ya Mbinga, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Ruvuma jana.
Ukifanywa utafiti wa kugundua upatikanaji wa makaa ya mawe kabla ya kuanza uchimbaji.
Makaa yakichekechwa na kupatikana makaa bora na mabaki kuwekwa mahala maalum palipoandaliwa ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.
Magari yakiwa mgdini chini yakiendelea na kazi ya uchimbaji wa Makaa ya mawe hayo ambayo soko lake kubwa limekuwa ni nje ya nchi kama Zambia, Ghana na kwingineko.
Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal (katikati) akiwa na Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma (kushoto) na Mke wa Mbunge wa Mbinga, wakati walipotembelea shughuli hiyo ya uchimbaji.
Sufianimafoto, naye hakusita kupiga picha ya kumbukumbu mahala hapa muhimu kwenye utajiri mkubwa wa Taifa la Tanzania.

Post a Comment

 
Top