Menu
 


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi wa soko la sido Mwanjelwa jijini Mbeya, ataka watendaji wabovu kuondolewa ili kuweka heshima kwa serikali.
*****
Habari na Mwandishi wetu
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa ametoa msaada wa mashine ya kuangua vifaranga vya kuku yenye thamani ya Shilingi milioni nne kwa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Kyela.

Akikabidhi msaada huo Mbunge huyo amesema maisha ya wanawake lazima yabadilike kutoka katika hali ya utegemezi na kuanza kuzisaidia familia zao kupitia jitihada zao wenyewe kupitia miradi ya mbalimbali.

Dakta Mwanjelwa amesema ni wakati kwa wanawake kutambua fursa za kimaendeleo zilizopo ikiwemo kujiunga katika Vikundi vya wajasiriamali ili kuwarahisishia wadau kuweza kuwasaidia.

Akipokea msaada huo Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya, Tabu Lugwesa aliwaomba wadau wengine kusaidia jumui za wanawake ili waweze kujikomboa dhidi ya utegemezi na kuwataka wanawake walipatiwa msaada huo kujituma na kuutumia msaada huo kama ulivyokusudiwa.

Post a Comment

 
Top