Menu
 

Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Athaanas Kapunga leo amewakimbia waandishi wa habari waliotaaka kumhoji juu ya mgomo wa wafanyabiashara katika soko la Soweto jijini hapa
Baada ya meya  huyo kukamilisha shughuli ya kuzungumza na wafanyabiashara na kutembelea miundombinu ya soko hilo wanahabari walimfuata wakitaka kuzungumza naye lakioni mmoja wa maafisa aliokuwa ameambatana nao Odas Aron akawaambia amesema atazungumza nao katika ofisi za jiji anakoelekea muda huo.

Wanahabari hao chapchap walitafuta usafiri binafsi na kuanza kufukuzia msafara wa meya lakini kutokana na foleni hawakujua kama walipigiwa chenga wapi na maskini wakaendelea na safari hadi ofisi za jiji na kuambulia patupu.


Baada ya kuuliza waliambiwa msafara huo haujafika ofisini hapo na ndipo ikawalazimu wanahabari kusubiri mpaka waluipokata tamaa,na hata walipojaribu kupiga namba za simu za Meya hazikupatikana huku ofisa aliyewapa maelezo kuwa Meya angezungumza nao ofisini kwake akiwa hapokei simu. 

Post a Comment

 
Top