Menu
 
Pichani ni Kete  za madawa ya kulevya.
*******
Habari na Mwandishi wetu.
Mapinduzi Magalasi mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Uyole jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kukutwa na bangi kete ishirini na sita.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakim mkazi Francis Kishenyi mwanasheria wa serikali Achilesi Mlisa amesema Agosti 22 2011 maeneo ya Uyole mshitakiwa alikutwa na kete 26 za bangi kinyume na kifungu cha sheria namba 12 (d) sura 95 marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo mshitakiwa amekana shitaka hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa mdhamini mwenye fedha shilingi laki mbili na barua kutoka kwa mtendaji na kesi hiyo itatajwa tena Februari 21 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top