Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashid Mtila (35), mkazi wa Kata ya Manga jijini Mbeya amekutwa amefariki chumbani kwake.

Mwili wa marehemu umegunduliwa na watu wawili waliokuwa wakienda kupata pombe za kienyeji katika moja ya nyumba iliyopo katika eneo hilo maarufu kama Jua Kali  Mwanjelwa, majira ya saa sita mchana Februari 19 siku ya jumapili.

Kwamujibu wa Balozi wa mtaa huo Bwana Godwini Kitwika alitoa taarifa kwa Diwani wa kata hiyo ya Manga mheshimiwa  Daniel Mwakisyala ambapo alitoa taarifa katika kituo cha polisi cha Mwanjelwa.

Pia marehemu alikuwa akiishi peke yake na siku mbili zilizopita na alianguka hivi karibuni katika kituo cha mabasi cha Mwanjelwa kwa kile kilichodhaniwa kuwa ni ugonjwa wa kifafa na siku hiyo alianguka mara tatu hali iliyomlazimu kwenda kupumzika chumbani kwake.

Hivyo kutokana na ukata wa maisha vijana wa mtaa huo walipitisha mchango wa dharura kwa ajili yakupata shuka ili kumuhifadhia marehemu huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Advocate  Nyombi ameruhusu mwili wa marehemu kuchukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya mazishi.

Post a Comment

 
Top