Menu
 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
***** 
Habari na Mwandishi wetu.
Jeshi la polisi Mkoani Mbeya lina mshikilia Basi Joseph mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Uyole kwa tuhuma za kuvunja stoo ya Songea Santom na kuiba mashine nane zenye thamani ya shilingi milioni kumi na nane laki saba na elfu tisini.

Akiongelea kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema mtuhumiwa alichimba ukuta wa nyuma ya stoo kisha kaingia ndani na kuiba mashine aina ya Sihil.

Aidha amesema mtuhimiwa alikuwa akifanya kazi ya kutunza stoo ya kampuni hiyo na kwamba mara baada ya tukio kutokea walinzi waliokuwa wakilinda ofisi za kampuni hiyo walitoroka mara baada ya tukio kutokea.

Post a Comment

 
Top