Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Jeshi la polisi mkoa wa Rukwa linamshikilia Epharimu Mwakabana mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa Chanji halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa tuhuma za kumuua mke wake baada ya kumfumania.

Tukio hilo la mauaji limetokea jana majira ya saa tatu za usiku nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo inadaiwa marehemu Bi.Fatuma Hasani na mtuhumiwa walikuwa wametengana na kwamba mtuhumiwa Bwana Mwakabana baada ya kumwona mke wake akiwa na mwanaume mwingine siku moja kabla ya tukio alimwita marehemu nyumbani kwake ili wazungumze lakini baada ya marehemu kufika lianza kupigwa hadi kufa na kisha mwili wake kutupwa barabarani jirani na kanisa la Katoliki.

Bi.Veronika Jackson amesema ameuona mwili wa marehemu leo hii majira ya saa kumi na mbili za asubuhi wakati akieda kanisani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Isuto Mantage amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mume wa marehemu  Epharimu Mwakabana na mwanae Winifrida Mwakabana wanashikiliwa kwa tuhuma za kusababisha mauaji hayo.

Post a Comment

 
Top