Menu
 


Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mwalimu Yusuph Mwamiko (55) wa Shule ya msingi Isimba iliyopo Kijiji cha Masoko, Kata ya Makwale wilaya ya Kyela mkoani Mbeya amejikuta yupo matatani baada ya kufukua kaburi la kaka yake aliyefariki Februari 2010, kisha kuzikwa nyumbani kwake ambapo mwalimu huyo alirithi mji huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho amesema Bwana Nicodemus Mwakasungula (41), amesema amesema tukio hilo limetokea katika Kitongoji cha Masoko kijiji cha Bwato majira ya saa 10 jioni hivyo alitoa taarifa polisi ambapo alikamatwa majira ya saa 11 jioni.
Amesema mwalimu Mwamiko kwa kushirikiana na Mganga wa kienyeji aliyetokea Ipinda walifukua kaburi la kaka wa mwalimu marehemu British Mwamiko aliyefariki  Februari 2010, ambapo mganga huyo alidai marehemu alizikwa na vitu katika miguu yake, ambayo ilivikwa viatu, na vitu ambavyo vilikuwa vinasababisha ugumu wa maisha (kiuchumi) na pia kuleta vifo katika ukoo wao na mpaka sasa watu 9 wamefariki hivyo kuzua hofu katika ukoo wao.
Shuhuda wa karibu Bwana Stephen David (28) amesema mwalimu Mwamiko ameshangaza kwa tendo hilo ambapo wakishirikiana na mganga huyo walifukua miguu katika kaburi hilo na kutoa vitu ambavyo hakuvielewa na hilo lilisababisha kutoa taarifa kwa uongozi wa serikali na walichukua hatua za kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na kufika na kumchukua mwalimu na mganga huyo wa kienyeji kwa mahojiano.
Imani za kishirikina zimehusishwa na tukio hilo ambapo uchunguzi unaendelea kufanyika ili kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo na wakati wowote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Post a Comment

 
Top